Sayyid Swafi ametembelea chuo kikuu cha Al-Ameed na amegagua mfumo wa elimu na ufundishaji

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ametembelea chuo kikuu cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu kwa ajili ya kukagua mfumo wa elimu na ufundishaji katika chuo hicho, hususan wakati huu ambao wanafunzi wa chuo wanafanya mitihani, sambamba na kuangalia mradi wa ujenzi wa upanuzi wa chuo hicho unaofanywa kwa sasa.

Amepokelewa na rais wa chuo Dokta Muayyad Gazali na wasaidizi wake, wamejadili hali ya masomo kwa wanafunzi wa chuo, pamoja na mitihani wanayo fanya na maandalizi yaliyofanywa na chuo, ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Hali kadhalika wamezungumza kuhusu ujenzi unaofanywa na chuo, na mambo mengine ya kielimu na kiutawala.

Mwishoni mwa ziara hiyo Mheshimiwa Sayyid Swafi amepongeza kazi nzuri inayofanywa na kuwataka waendelee na kazi hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: