Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa mafunzo ya mbinu za ukarabati wa mali-kale, kwa lengo la kujenga uwezo wa watumishi wa sekta ya ukarabati wa mali-kale.
Mkufunzi wa semina hiyo ni Ustadh Muhammad Qassim kutoka kitengo cha turathi katika wizara ya utamaduni ya Iraq, ujio wake ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzowefu.
Rais wa kitengo cha makumbusho Ustadh Swadiq Laazim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Makumbusho ya Alkafeel imepata maendeleo makubwa, ili kuwafanya wahudumu wake waendane na maendeleo hayo, tunatoa semina kwa wahudumu wa idara ya maabara na matengenezo”.
Akaongeza kuwa: “Mkufunzi wa semina hii itakayo dumu kwa muda wa siku tano ni Ustadh Muhammad Qassim kutoka idara ya turathi, mafunzo yanatolewa kwa njia ya nadhariyya na vitendo kuhusu ukarabati wa mali-kale, wanafundishwa mbinu za kielimu za kutengeneza sehemu zilizo haribika kwenye mali-kale”.
Akamaliza kwa kusema: “Tunatarajia kuendelea kutoa semina za aina hii, kwani zina mchango mkubwa wa kutunza mali-kale na kurudisha uhai wake, sambamba na kuongeza uwezo wa watumishi wa sekta hii, bila kusahau umuhimu wa kuendelea kujifunza na kuongeza uwezo sambamba na maendeleo ya kielimu kwenye sekta hii”