Multaqal-Qamaru inapanua harakati zake kifikra na kijografia

Maoni katika picha
Kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinapanua wigo wa kutoa huduma kitamaduni na kijamii, mara hii wameingia katika mji wa Baldaruuz mkoani Diyala, hii ni mara ya kwanza watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kuwasiri kwenye mji huo.

Kitengo hicho kwa kushirikiana na kikosi cha (maendeleo) wanafanya warsha ndani ya husseiniyya ya Zaharaa (a.s), chini ya usimamizi wa muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Hisham Shimri.

Warsha imefunguliwa kwa mhadhara uliotolewa na makamo mkuu wa kituo Ustadh Farasi Shimri, wenye anuani isemayo (kujitambua na athari yake katika mabadiliko) akaeleza umuhimu wa mtu kujitambua.

Halafu akaongea mkufunzi wa kituo Ustadh Hassan Jawadi mada isemayo (majukumu ya mtu katika jamii), akabainisha nafasi ya kijana katika kubadilisha jamii na majukumu yao, akatahadharisha hali ya mtu kujisahau na kutotekeleza wajibu wako.

Ratiba ilihitimishwa kwa pongezi nyingi alizopewa mkuu wa program hii Dokta Muhammad Tamimi pamoja na viongozi wengine, wakasifu kazi kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kufundisha maadili mema kwa vijana wa Iraq.

Kumbuka kuwa Multaqal-Qamaru ni mradi wa kutoa mafunzo ya kielimu na kitamaduni kwa makundi ya watu tofauti, kwa lengo la kujenga jamii inayo jitambua na kuishi vizuri kwa maelewano na mshikamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: