Muitikio mkubwa wa kufunga ndoa katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshuhudia muitikio mkubwa wa watu wanaokuja kufunga ndoa, kufuatia kumbukumbu ya ndoa ya nuru kwa nuru, kijana wa kihashimiyya ambaye Mtume (s.a.w.w) alimsifu kwa kusema: (Hakuja kijana ispokua Ali wala jambia ispokua Dhul-fikaar), na nuru ya pande lake takatifu, anasema (s.a.w.w): (Fatuma ni sehemu ya mwili wangu atakae muudhi atakua kaniudhi mimi).

Idara ya ndoa chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kila mwaka tarehe kama hizi hushuhudia idadi kubwa ya watu wanaokuja kufunga ndoa, kwa ajili ya kutabaruku na ndoa ya kiongozi wa waumini na Fatuma Zaharaa (a.s).

Idara huanza kupokea watu wanaokuja kufunga ndoa tangu asubuhi, asilimia kubwa ya watu wanaokuja kufunga ndoa ni wale waliochelewesha ndoa zao kwa ajili ya kusubiri tarehe hizi tukufu, ili wafunge katika siku tukufu na mahala patakatifu wakati wa kuadhimisha tukio takatifu.

Ndoa zinafungwa kwa mujibu wa sheria mbele ya walii wa mwanamke na wasimamizi wa mwanaume pamoja na mashahidi, na inaongozwa na mmoja wa masayyid au mashekhe ambao ni watumishi wa kitengo hicho, sambamba na kuwaombea dua ya maisha mema ya ndoa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: