Warsha elekezi kwa wanaskaut wa Alkafeel

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya imefanya warsha elekezi kwa watoa huduma wa kujitolea wapatao (74), watakao shiriki kutoa huduma za kiafya kwa mazuwaru kwenye vituo vya afya, kwa lengo la kuongeza uwezo wao na kuwapa uzowefu wa kutoa huduma hiyo kwa vitendo.

Warsha hii ni sehemu ya ratiba za hema za watoa huduma wa kujitolea chini ya ukufunzi wa Sayyid Muhammad Mussawi kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nayo ilikua na sehemu mbili:

Kwanza: warsha ya mjadala wa wazi kuhusu kazi njema na matokeo yake, kunafaida nyingi anazopata mtu anayefanya kazi njema katika maisha yake, kuna shuhuda nyingi za kisheria zinazo onyesha matunda ya kufanya wema, mtu anayedumu katika kufanya wema hupata faida nyingi, huwa ni sababu ya kupendwa na Mwenyezi Mungu mtukufu, jambo lolote unalofanya kwa ajili ya kusaidia watu Mwenyezi Mungu anakulipa na kukuandika katika orodha ya waja wema, zikatajwa aya na hadithi za Mtume na Ahlulbait (a.s) nyingi zinazo thibitisha jambo hilo.

Pili: warsha ya pili ilikua inahusiana na ya kwanza, anuani yake ilikua inasema (Utukufu wa kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein –a.s- pamoja na ubora na karama anazopata mtumishi wa Hussein kwa kufuata tabia na mwenendo wa maasumina –a.s-).

Mwisho wa warsha hiyo kulikua na maswali mbalimbali kutoka kwa washiriki, mhadhiri aliyajibu na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipo hitajika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: