Ugeni wa walimu na waandishi wa habari kutoka chuo kikuu cha Dhiqaar umetembelea Atabatu Abbasiyya na kuangalia miradi mbalimbali inayofanywa na Ataba pamoja na huduma zinazo tolewa.
Makamo rais wa kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Ahmadi Swadiq amesema: “Ziara hii imefungua mlango wa mawasiliano na ushirikiano baina ya Ataba na chuo cha Dhiqaar”.
Swadiq akasema: “Ugeni huo umetembelea miradi inayofanywa na Ataba tukufu, na kushuhudia mafanikio yaliyo fikiwa pamoja na huduma zinazo tolewa kwa jamii”.
Akabainisha kuwa: “Kuna matokeo mazuri sana kufuatia huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya kwa raia wa Iraq, wameshuhudia hayo baada ya kuangalia miradi iliyofanywa na huduma zilizotolewa ndani ya kipindi kifupi”.
Ustadh Khafaji mkufunzi wa chuo kikuu cha Dhiqaar amesema: “Ziara yetu katika Atabatu Abbasiyya inatokana na mualiko wao, tumeona ukomavu wa Ataba tukufu katika kufanya miradi ya kimkakati ukiwemo mradi wa habari”.
Akaongeza kuwa: “Ni jambo zuri kwa Ataba tukufu kuchukua wanahabari kutoka sehemu tofauti na kujadili mustaqbali wa taifa katika sekta mbalimbali”.
Akasema: “Miradi inayofanywa hivi sasa na Atabatu Abbasiyya ni muhimu sana katika sekta ya viwanda, biashara, afya na huduma tofauti”.
Akasisitiza kuwa: “Kazi kubwa inayofanywa na Ataba tukufu ni fahari pia kwa taasisi zingine”.