Idara ya shule za Dini za wasichana, inafanya mashindano ya Alhaji mdogo kwa Watoto wenye miaka saba hadi kumi na tatu, kufuatia kukaribia msimu wa hija kwa lengo la kuwajulisha ibada hiyo takatifu.
Kiongozi wa idara hiyo bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano hili linalenga kumtambulisha mtoto ibada ya hija pamoja na vigawanyo vyake na matendo ya sunna na wajibu katika ibada hiyo, kuanzia Ihraam hadi kupiga mawe kwa kuzingatia umri wa walengwa”.
Akaongeza kuwa: “Mtoto anayependa kushiriki anaweza kuangalia faili la utambulisho na kuingia kwenye mashindano, kutakuwa na zawadi za washindi pamoja na kugawa vyeti vya ushiriki kwa wote”.
Kumbuka kuwa idara ya shule za Dini Alkafeel hufanya mashindano mbalimbali katika kipindi cha mwaka mzima, kwa wasichana wenye umri tofauti, kwa lengo la kuongeza elimu na maarifa kwa makundi hayo.