Harakati za wiki ya kilimo zinachechemua bidhaa za nyuki za Alkafeel

Maoni katika picha
Awamu ya kumi na mbili ya maonyesho ya wiki ya kilimo yanayo fanywa hivi sasa kwenye viwanja vya maonyesho ya kimataifa Bagdad, kikosi cha walinaji wa Alkafeel kimeshiriki na kuwa kivutio kikubwa kwa watu wanaotembelea maonyesho hayo, kushiriki kwenye maonyesho haya ni muendelezo wa ushiriki wa maonyesho mbalimbali, tumeonyesha aina tofauti za asali.

Kiongozi wa kikosi hicho Mhandisi Hassanaini Muhammad ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ushiriki wa maonyesho kama haya unafaida nyingi, miongoni mwa faida hizo ni kutambulisha bidhaa tunazo zalisha pamoja na kubadilishana mawazo na walinaji wengine wa Iraq wanaoshiriki kwenye maonyesho, kuhusu namna ya kuboresha sekta hii muhimu hapa nchini”.

Akaongeza kuwa: “Tumeonyesha aina mbalimbali za asali halisi, iliyo hifadhiwa kisasa zaidi, miongoni mwa aina za asali tulizo nazo ni: Kabtuz, Kukatiil, Barsim, Matbaluur, Sidri, Maua tofauti, aidha tumeonyesha mbegu ambazo hutumika kutengeneza (Akbaru) au kuongeza thamani ya asali tiba ambayo hutibu maradhi mengi yenyewe au kwa kuchanganywa na kitu kingine”.

Akafafanua kuwa: “Tawi letu limepata muitikio mkubwa kutoka kwa watu wanaokuja kutembelea maonyesho haya, akiwemo Waziri wa kilimo Mheshimiwa Muhammad Karim Alkhafaji aliyepongeza ushiriki wetu na kufurahishwa na bidhaa tulizo nazo”.

Kumbuka kuwa maonyesho haya Ataba imeshiriki kupitia (Shirika la kibiashara Alkafeel, shirika la Khairul-Juud, shirika la Nurul-Kafeel linalo zalisha bidhaa za chakula cha binaadamu na wanyama, shirika la Liwaau Al-Aalamiyya), chini ya maelekezo ya Atabatu Abbasiyya kwa lengo la kuchangia uzalishaji wa ndani, na kuonyesha bidhaa zetu, aidha ushiriki ni sehemu muhimu ya kujenga mawasiliano na taasisi zingine pamoja na kuona maendeleo yaliyopo katika sekta hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: