Kamati ya maelekezo na msaada inaendelea na ziara zake

Maoni katika picha
Kamati ya maelekezo na msaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea na ziara zake pamoja na kusaidia wanajeshi na wapiganaji wa kujitolea Hashdu-Sha’abi, safari hii wametembelea vikosi vya mashariki ya Ambari.

Kiongozi wa kamati hiyo Shekh Haidari Aaridhwi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara hii ni miongono mwa mfululizo wa ziara zetu tulizo anza kufanya siku za kwanza baada ya kutolewa fatwa na Marjaa Dini mkuu ya kulinda taifa la Iraq na maeneo matakatifu, tumeshatembelea vikosi vya wapiganaji mbalimbali”.

Akaongeza kuwa: “Safari hii tumetembelea Liwaau ya pili ya kikosi cha Imamu Ali (a.s) kundi la kwanza, wanaolinda amani katika eneo la Swaqlawiyah na Abu-Shajal mashariki ya Ambari, tumewafikishia dua na salam kutoka kwa Marjaa Dini mkuu na ndugu zao watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuwapa baadhi ya usia na maelekezo yanayo wapa moyo na kuwajengea ari, aidha tumewapa pia baadi ya vitu muhimu kwao na zawadi za kutabaruku kutoka ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Wapiganaji wamesifu na kuishukuru Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana nao wakati wote kwenye uwanja wa vita na katika maeneo yaliyo kombolewa, wakasema kuwa jambo hilo linawapa moyo zaidi wa kuendelea kupambana na kuwa ngome imara dhidi ya kila mtu anayetaka kuharibu amani na utulivu wa taifa hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: