Kufungua mlango wa kushiriki awamu ya tatu ya program ya (Rafiki bora)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya, kimefungua mlango wa kushiriki katika awamu ya tatu ya program iitwayo (Rafiki bora), na imetoa wito kwa kila anayetaka kuongeza maarifa aje kushiriki.

Mkuu wa kituo bibi Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika program hii na muitikio ulioshuhudiwa katika awamu zilizo pita, tumeona tuendelee na program hii inayo saidia kukuza nafasi ya mwanamke katika harakati za Dini, na kukuza vipaji na ubunifu kwa wanawake”.

Akaongeza kuwa: “Mada ya program hii inahusu kuandika (malezi ya familia) nao ni mfululizo wa maandalizi ya kitamaduni, inalenga masomo ya Maisha ya ndoa na familia, tunatoa mafunzo kupitia maswali ya kuchagua, tutachagua washindi watatu kupitia kura, zowezi hili litadumu kwa muda wa siku kumi na tano (15)”.

Kumbuka kuwa program inalenga kuimarisha harakati za wanawake na kuongeza maarifa kwa kuwashajihisha kusoma na kufanyia kazi wanayo yasoma katika maisha yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: