Nadwa kuhusu uwelewa wa kujenga familia katika Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi ka wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya nadwa yenye anuani isemayo: (Ujenzi wa familia katika Qur’ani.. ndoa ya nuru mbili kama mfano), kufuatia kumbukumbu ya kukutana nuru ya Alawiyya na Fatwimiyya, ndani ya jengo la Maahadi katika mkoa wa Najafu.

Mtoa mada wa nadwa hiyo alikua ni Ustadhat wa Fiqhi na mbobezi wa ushauri nasaha wa kidini bibi Zainabu Swadiq, ameongea mambo mengi, akianzia na ndoa ya nuru mbili, ndoa ya mfano katika maisha ya ndoa na taa liangazalo njia ya uongofu na usawa, hakika Maisha yao ya ndoa yanafaa kuigwa na kila mtu anayependa haki na kupata daraja kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, akatoa Ushahidi wa Qur’ani na hadithi za Mtume pamoja na Ahlulbait wake (a.s).

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi akasema kuwa: “Tukio la kiongozi wa waumini kumuoa Fatuma Zaharaa (a.s), linamafunzo makubwa ya namna ya kujenga familia ya kiislamu, aidha ni kielelezo halisi cha mafundisho ya Qur’ani na uislamu mtukufu, hivyo Maahadi imeamua kufanya nadwa ya kuzungumzia ndoa hiyo na kuilinganisha na hali halisi ya familia zetu za sasa”.

Nadwa imehudhuriwa na walimu pamoja na wanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu, kwa kuzingatia taratibu zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: