Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil imefanya semina ya kuwajengea uwezo walimu wake

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya inafanya semina ya kujengea uwezo walimu wake, wamefundishwa masomo mengi ikiwa ni pamoja na hukumu za usomaji wa Qur’ani, tajwidi na njia za ufundishaji.

Semina imefanywa ndani ya jengo la Maahadi lililopo katika mji wa Hilla makao makuu ya mkoa wa Baabil, imewahusu walimu wa Maahadi wanaofundisha katika kitongoji cha Abugharqi na Mahanawiyya kaskazini mashariki ya mkoa, kwa lengo la kukuza uwezo wa walimu kupitia semina za Qur’ani za majira ya kiangazi (joto).

Nayo ni muendelezo wa semina za walimu, tawi linazaidi ya walimu (300), wanaofundisha masomo tofauti kwa wakazi wa kitongoji hicho.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil hufanya semina za Qur’ani na masomo mengine kwa wanajamii ili kujenga utamaduni wa kushikamana na vizito viwili.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya kupitia matawi yake tofauti, hufanya program mbalimbali za Qur’ani ndani na nje ya mkoa wa Karbala, pamoja na kuendesha semina za Qur’ani mfululizo kwa lengo la kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: