Amani iwe juu ya Baaqir-Ilmu ba’ada Nabiyyiin

Maoni katika picha
Leo ni siku ya kumbukumbu ya mmoja kati ya misiba ya Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao, ni siku aliyokufa Imamu Muhammad Baaqir (a.s) Imamu wa tano mtakatifu, miongoni mwa Maimamu waliobashiriwa na Mtume (s.a.w.w), alikufa mwezi saba Dhulhijja mwaka wa (114) hijiriyya.

Inasemekana alipewa sumu na Ibrahim mtoto wa Walidi mtoto wa Abdulmaliki, kifo chake kilitokea wakati wa utawala wa Hisham bun Abdulmaliki, Imamu Swadiq (a.s) akasimamia maziko yake na kumzika katika makaburi ya Baqii katika mji wa Madina, akazikwa karibu na kaburi la Ammi wa baba yake Imamu Hassan Almujtaba (a.s), pamoja na kaburi la baba yake Imamu Ali Zainul-Aabidina (a.s), alimuhusia mwanae Jafari (a.s) amvishe nguo aliyokua anaswalia siku za Ijumaa, na amvishe kilemba chake, baada ya kumzika kaburi lake aliinue kwa urefu wa vidole vine.

Miongoni mwa mambo muhimu aliyosifika nayo Imamu Abu Jafari (a.s) ni kufundisha elimu kwa watu, watu wengi walisoma kwake, alikua na elimu kubwa akiwa bado kijana mdogo, aliacha usia kwa mwanae Imamu Jafari (a.s) awagharamie watu waliokua wanaandika hadithi walizo sikia kutoka kwake hadi watakapo maliza, wanafunzi walio hitimu kwake walikua watu bora katika umma, wanachuoni wakubwa, Imamu Jafari (a.s) aliwaambia wafuasi wake kua: Wafuasi wa baba yangu walikua bora zaidi yenu, walikua ni karatasi isiyo na miba na nyie ni miba isiyo na karatasi.

Ulimwengu wa kiislamu ulinufaika sana na elimu yake, manufaa hayakuishia katika zama zake peke yake, bali yaliendelea hadi katika zama zingine, elimu ilikua sana katika jamii ya waislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: