Majlisi ya kuomboleza kifo cha Baaqirul-Uluum

Maoni katika picha
Ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imefanywa majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir (a.s), kwa muda wa siku mbili mfululizo, kila siku ikiwa na mhadhara mmoja uliohudhuriwa na mazuwaru pamoja na watumishi wa malalo hiyo takatifu.

Majlisi ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha Sayyid Adnani Jalukhani Mussawi kutoka kitengo cha Dini akapanda mimbari na kuongea historia ya Imamu (a.s), na mambo yaliyotokea wakati wa uhai wake, pamoja na kazi kubwa iliyofanywa na Imamu (a.s) katika kubaini haki na batili.

Hali kadhalika akaongea kuhusu mambo yaliyo mtokea Imamu Baaqir (a.s), yakiwemo yanayo sikitisha kama yale aliyoshuhudia katika uwanja wa Karbala, na yaliyojiri kwa babu yake Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake.

Majlisi ikahitimishwa kwa kueleza tukio la kifo cha Imamu Baaqir (a.s), na kufananishwa na yaliyojiri katika uwanja wa Karbala kihistoria, pamoja na madhila waliyofanyiwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) yasiyokua na mfano katika historia.

Kumbuka kuwa Imamu Baaqir (a.s) alizaliwa mwezi wa Rajabu mwaka wa (57) hijiriyya katika mji wa Madina, akafa mwezi (7 Dhulhijjah 114h) kwa sumu aliyopewa na Ibrahim bun Walidi bun Hisham bun Abdulmaliki wakati wa utawala wake, akazikwa (a.s) katika makaburi ya Baqii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: