Mawakibu zinaomboleza kifo cha Imamu Baaqir (a.s)

Maoni katika picha
Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) tangu asubuhi ya leo mwezi saba Dhulhijjah, imeshuhudia kuwasili mawakibu nyingi za waombolezaji kutoka sehemu tofauti za mji wa Karbala, zikija kuomboleza kifo cha Imamu Baaqir (a.s).

Huo ni utamaduni wa mawakibu za watu wa Karbala, zimekuja kutoka sehemu tofauti za mji huu zikiwa zimebeba jeneza la kuigiza la Imamu aliyeuwawa kwa sumu, wakaingia katika malalo ya Imamu Hussein na malalo ya ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kuwapa pole pamoja na Imamu wa zama msubiriwa (a.f).

Matembezi hayo yalianzia katika moja ya barabara inayo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuingia katika malalo hiyo takatifu, kisha kuelekea katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) wakipita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimeweka utaratibu unao endana na mazingira ya sasa, mawakibu zinatembea bila kusababisha usumbufu wowote kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: