Tambua utukufu wa usiku na mchana wa siku ya Arafa na ibada zake muhimu

Maoni katika picha
Usiku wa Arafa:

Ni usiku wa Tisa wa mwezi wa Dhulhijjah, nao ni usiku mtukufu, usiku wa kuomba dua na toba katika usiku huo hukubaliwa, dua hujibiwa, mtu anayefanya ibada katika usiku huo huandikiwa thawabu sawa na aliyefanya ibada miaka mia moja na sabini, kuna ibada nyingi zilizo suniwa:

Kwanza: Usome dua hii: (Allahumma yaa shaahida kulla Najwa wa maudhia kulla shakwa…) Mafatihul-Jinaan ukurasa wa 333, imepokewa kuwa atakaesoma dua hiyo katika usiku wa Arafa au usiku wa Ijumaa Mwenyezi Mungu atamsamehe.

Pili: Asome mara elfu moja tasbihaat kumi: (Subhana Llahi qabla kulla ahad, wa subhana Llahi baada kulla Ahad…) Mafatihul-Jinaan ukurasa wa 341.

Tatu: Usome dua (Allahumma man ta’abba-a wa tahayya-a wa a’dda wa sta’adda liwifadatin ila makhluqi rajaa rafadahu wa twalaba naailahu…) Mafatihul-Jinaan ukurasa wa 62.

Nne: Usome ziara ya Imamu Hussein (a.s) Mafatihul-Jinaan ukurasa wa 547.

Mchana wa Arafa:

Mchana wa tisa katika mwezi wa Dhulhijjah nao ni sikukuu kubwa japokua haiitwi kama sikukuu, ni siku ambayo Mwenyezi Mungu amewataka waja wake wamtii na kumuabudu, na kawaandalia wema na ukarimu wake, katika siku hiyo shetani huwa dhalili, mnyonge, mwenye hasira kushinda siku zote.

Imepokewa kuwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s) katika siku ya Arafa alisikia muombaji anaomba mtu, akasema: Umeangamia, unaomba asiyekua Mwenyezi Mungu katika siku hii?! Siku ambayo hadi mtoto aliyetumboni mwa mama yake hufikiwa na rehema ya Mwenyezi Mungu na kufurahi.

Siku hii inaibada nyingi:

Kwanza: Kuoga.

Pili: Kumzuru Hussein (a.s) nayo ni ibada muhimu sana, Mwenyezi Mungu huwaangalia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) siku ya Arafa kabla ya kuwaangalia waliosimama katika uwanja wa Arafa, Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Atabae zuru kaburi la Hussein (a.s) katika siku ya Arafa, Mwenyezi Mungu atamuandikia thawabu za hijja laki moja alizofanya pamoja na Imamu wa zama, na umra laki moja alizofanya na Mtume (s.a.w.w), na kuacha huru watumwa laki moja, na kutoa farasi laki moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamuita mja wangu mkweli ameamini ahadi yangu, na Malaika watasema: Fulani mkweli ametakaswa na Mwenyezi Mungu juu ya arshi yake).

Hivyo siku ya tisa katika mwezi wa Dhulhijjah ni sikukuu kubwa japokua haiitwi kama sikukuu, ni siku ambayo Mwenyezi Mungu amewataka waja wake wamtii na kumuabudu, na kawaandalia wema na ukarimu wake, katika siku hiyo shetani huwa dhalili, mnyonge, mwenye hasira kushinda siku zote.

Tatu: Baada ya swala ya Alasiri kabla ya kuanza kusoma dua za Arafa, uswali rakaa mbili chini ya mbingu, na kukiri mbele ya Mwenyezi Mungu dhambi zako, ili Mwenyezi Mungu akusamehe, kisha anza kusoma dua za siku ya Arafa kama zilivyo pokelewa.

Nne: Kufunga ni sunna kwa yule ambaye funga haitamdhofisha katika dua.

Tano: Usome dua iliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): (Subhana man fii samaai arshuhu, subhana lladhi fil-ardhi hukumuhu…) Mafatihul-Jinaan ukurasa wa 339.

Sita: Usome dua ya Imamu Hussein (a.s): (Alhamdulillahi ladhii laisa liqadhwaaihi daafiu, wala liatwaaihi maaniu, wala kasun’ihi sunu’u swaani’u, wa huwal-jawaadul-waasi’u…) Mafatihul-Jinaan 343.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: