Mwezi tisa Dhulhijjah ni siku aliyouwawa kishahidi balozi wa Imamu Hussein Muslim bun Aqiil (a.s)

Maoni katika picha
Wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika siku kama ya leo mwezi tisa Dhulhijjah kila mwaka wanakumbuka kifo cha Muslim bun Aqiil (a.s) balozi wa Imamu Hussein (a.s) kwa watu wa Kufa, alimtuma kwenda huko baada ya kupokea barua nyingi zikimuomba aende katika mji huo kuwaokoa na udhalimu wa bani Umayya.

Riwaya zinaonyesha Muslim alipowasili Kufa alipokewa na watu wengi kwa furaha na bashasha, akawasomea barua ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), akawajulisha kuwa yuko tayali kufanya wanavyo taka kama watashikamana na ahadi zao na kufanya subira dhidi ya vitimbi vya adui wao, alipo wataka kula kiapo cha utii, watu wote walienda kula kiapo na kisema wako tayali, ndipo akamuandikia Imamu Hussein afanye haraka kuja, lakini watu wale walibadilika haraka sana wakakosa utukufu wa duniani na kufaulu katika Dini, yakamtokea Muslim katika mji wa Kufa kama yaliyo mtokea Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala, watu wakavunja ahadi zai na viapo vyao.

Ibun Ziyadi akatoa amri ya kusachi nyumba za Kufa moja baada ya nyingine, kumtafuta Muslim bun Aqiil (a.s), aliyekua amejificha katika nyumba ya mwanamke mpenzi wa Ahlulbait (a.s) aitwae (Twau’ah), Ibun Ziyadi alipotambua kuwa yupo katika nyumba hiyo alituma jeshi kwenda kumkamata, Muslim akapigana nao vita kali sana, hawakuweza kumkamata hadi walipo tumia hila na udanganyifu, wakampeleka akiwa mateka kwenye qasri la Ibun Ziyadi, Ibun Ziyadi akaamuru apandishwe juu ya qasri lake kisha akatwe kichwa na muili wake utupwe chini, upanga wa muovu ukatenganisha kichwa na muili wa Muslim bun Aqiil, akapata shahada na kuelekea kwa Mola wake, amani iwe juu yake shahidi wa kwanza aliyetolewa na Hussein (a.s), amani iwe juu ya muumini mliwazaji wa Imamu wake aliyeuwawa ugenini siku aliyo zaliwa na siku aliyo uwawa na siku atakayo fufuliwa kuwa hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: