Maahadi ya Qur’ani tukufu na Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) zinaendesha semina ya hukumu za usomaji wa Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu kwa kushirikiana na kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya semina ya hukumu za usomaji wa Qur’ani na matamshi ya herufi, kwa ushiriki wa watumishi (15) wa Ataba tukufu.

Semina hiyo inafanywa ndani ya Magaam ya Imamu Hujjat (a.s) chini ya ukufunzi wa Shekh Ali Rawii mmoja wa walimu wa Maahadi ya Qur’ani ambaye amefundisha hukumu za usomaji wa Qur’ani tukufu kwa nadhariyya na vitendo siku zote za semina.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya hutoa semina za Qur’ani kwa makundi yote ya watu katika jamii.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia matawi yake huendesha program mbalimbali za Qur’ani ndani na nje ya mkoa wa Karbala, pamoja na miradi tofauti ya Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: