Mwezi kumi Dhulhijja katika kila mwaka ni sikukuu ya Idul-Adh-ha, nayo ni kikukuu ya waislamu wote, kama ilivyo kuja katika dua: (Ewe Mola mimi nakuomba hifadhi karama na ziada… kwa haki ya siku hii, uliyofanya kuwa sikukuu kwa waislamu na Muhammad (s.a.w.w)).
Sikukuu hii imeitwa siku ya kuchinja; kwa sababu mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu wanafanya ibada ya kuchinja (ng’ombe au mbuzi/kondoo) katika eneo la Mina, baada ya kurudi kutoka Arafaat, Mwenyezi Mungu anasema: (Ili washuhudie manufaa yao na wataje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalum kutokana na walichoruzukiwa katika wanyama kuleni na muwalishe mafakiri).
Kutoka kwa Mufadhwil bun Omari anasema: Abu Abdillahi (s.a) aliniambia kuwa: (Itakapofika siku ya kiama, siku nne zitaenda kwa Mwenyezi Mungu kama biharusi anavyoenda kwa mumewe, nazo ni siku ya Fitri, siku ya Udh-hiya, siku ya Ijumaa na siku ya Ghadiir-Khum).
Amepokea Abu Mukhnifu kutoka kwa Abdurahmani bun Jundab kutoka kwa baba yake kwamba Ali (a.s) alihutubia siku ya Udh-hiya akasema: (Nakuusieni kumcha Mwenyezi Mungu, na mkithirishe kutaja mauti, nakutahadharisheni na dunia ambayo haijawahi kumstarehesha yeyote kabla yenu, wala haitabaki kwa ajili ya yeyote baada yenu, njia ya watu mliopo duniani ni ileile ya waliopita kabla yenu, tambueni kua inaelekea mwisho, wema wake umeisha, imetupa mgongo na kupiga ukelele wa mwisho,ukelele wa mauti, mambo yaliyokua matam sasa ni machungu, yaliyo kuwa masafi sasa ni machafu, kilicho baki sawa na unyevuvyevu wa maji kwenye chombo usiokua na faida yeyote, jiandaeni na safari, kusanyeni vitu vyenu, hakuna uhai utakaobaki, nafsi zote zitaenda kwa Mola wao, msidanganywe na shetani.
Muabuduni Mwenyezi Mungu katika siku za uhai wenu, wallahi lau mtakuwa wapole na kuomba dua pamoja na kujielekeza kwa Mwenyezi Mungu kwa mali na watoto mtuakuwa karibu nae na atakupandisheni daraja, na kukusameheni dhambi na mtastahiki pepo na rehema zake.
Tambueni kuwa hii ni siku tukufu iliyojaa baraka zake, kithirisheni kumtaja Mwenyezi Mungu, tegemeeni kupata thawabu kwa kufanya toba na kujikurubisha kwake, hakika hukubali toba ya waja wake na husamehe thambi naye ni mwingi wa rehema…)