Shirika la Nurul-Kafeel linazalisha bidhaa bora na linachangia uchumi wa taifa

Maoni katika picha
Mradi wa kuku ni miongoni mwa miradi muhimu ya shirika la Nurul-Kafeel, umechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha uzalishaji wa ndani, pamoja na kuongeza uchumi na kutoa ajira.

Kuhusu utendaji wa shirika hilo na jinsi linavyo zalisha bidhaa mkuu wa shirika la Nurul-Kafeel amesema: “Shirika la Nurul-Kafeel limeboresha uzalishaji wa nyama hapa nchini baada ya kuzalisha bidhaa hiyo nje ya nchi kwa miaka mingi”.

Akaongeza kuwa: “Hivi sasa kuku zinafugwa katika mkoa wa Karbala baada ya kujenga machinjio ya kisasa katika mji huo”.

Akaendelea kusema: “Hatua ya ufugaji huanzia katika kuchagua vifaranga bora vinavyo pewa chakula cha asili, ambacho hupelekea kuwa na nyama nzuri wanapo fikia umri wa kuchinjwa, kuku wanafugwa na watu waliobobea katika ufugaji huo, ambao huhakikisha usalama wao na kuwalinda na maradhi ya kuambukiza”.

Akasema: “Uchinjaji unafanywa na watu waliokamilisha masharti, huelekezwa kibla na kutajwa jina la Allah kwa kila kuku, sambamba na kufuata kanuni zote za uchinjaji kwa kukata mishipa minne kikamilifu, kwani hilo ni sharti la lazima katika uchinjaji”.

Akasema: “Kisha kuku hupelekwa katika hatua ya kunyonyolewa na kutolewa utumbo pamoja na kusafishwa maini na filigisi, kisha hupimwa kama ilikua na athari kwenye mifupa yake halafu huwekwa kwenye kifungashio akiwa mzima au vipande vipande”.

Akasisitiza kuwa: “Hatua ya mwisho hupimwa uzito wake na kuandikwa juu ya kifungashio na hapo huwa tayali kwa kupelekwa kwenye vituo vya mauzo vilivyopo sehemu tofauti hapa nchini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: