Zaidi ya watu elfu 33 wamefanyiwa ziara ya Arafa na Idi kwa niaba

Maoni katika picha
Idara ya taaluma na mitandao chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu imesema kuwa jumla ya watu (33,471) wamefanyiwa ziara ya Arafa na Idi kwa niaba kupitia ukurasa maalum uliopo katika toghuti ya kimataifa Alkafeel ambayo ndio toghuti rasmi ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema kuwa: “Tumepokea maombi ya ziara kupitia toghuti zote za Alkafeel za (Kiarabu – Kiengereza – Kifarsi – Kituruki – Kiurdu – Kifaransa – Kiswahili – Kijerumani), toghuti hizo zimepokea maombi mengi kutokana na mazingira ya sasa ambayo dunia inapitia pamoja na taifa la Iraq, yaliyopelekea watu wengi kushindwa kuja kufanya ziara”.

Akafafanua kuwa: “Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya wamefanya ibada hiyo ya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ambayo ni ziara ya siku ya Arafa na ibada zake pamoja na ziara ya siku ya Idi”.

Akabainisha kuwa: “Asilimia kubwa ya watu waliojiandikisha katika ukurasa wa ziara kwa niaba wanatoka katika nchi za: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistan, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuwait, Malezia, Australia, Aljeria, Baharain, Misri, Ujerumani, Islandi, Namsa, Yunani, Holandi, Tunisia, Denmak, Norwey, Qatar, Ubelgiji, Moroko, Afghanistani, Omani, Ekwado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijan, Qabrus, Finland, China, Ealend, Honkon, Japani, Umoja wa falme za kiarabu, Sudani)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: