Mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Tumegawa maelfu ya sahani za chakula katika ziara ya Arafa na Idi

Maoni katika picha
Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu umesema kuwa umegawa maelfu ya chakula katika ziara ya siku ya Araba na Idi, kwa mazuwaru wa malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kufuata mashari ya afya ili kuwalinda mazuwaru na wahudumu.

Rais wa kitengo Mhandisi Aadil Hamaami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara ya siku ya Arafa ni miongoni mwa ziara ambazo huwa tunagawa chakula kwa mazuwaru, tulianza kugawa tangu siku ya kwanza, mazuwaru walianza kumiminika kwa wingi siku ya mwezi tisa Dhulhijjah hadi siku ya mwezi kumi, tulipika chakula cha aina tofauti na tukagawa kupitia vituo maalum vya kugawia chakula, kilele cha mazuwaru ilikuwa ni usiku wa Idi na mchana wake”.

Akaongeza kuwa: “Tumegawa milo mitatu pamoja na (matunda, juisi na vinginevyo), kupitia vituo maalum vya ugawaji wa chakula bila kusababisha msongamano kwa mazuwaru wala usumbufu wowote”.

Kumbuka kuwa ni desrturi ya mgahawa huu kugawa chakula bure kwenye kila ziara inayo hudhuriwa na mazuwaru wengi, mazuwaru hupanga mistari miwili wakati wa kwenda kuchukua chakula, mstari wa wanaume na mwingine wa wanawake, imekua ikifanya hivyo pia katika matukio makubwa ya kidini, hadi umekua maarufu kwa kutoa huduma ya chakula kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: