Kuondoa uvimbe katika uso wa mgonjwa kutoka mkoa wa Dhiqaar

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa kiiraq katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abasiyya tukufu, limefanikiwa kuondoa uvimbe katika uso wa kijana mwenye umri wa zaidi ya miaka thelathini kutoka Dhiqaar.

Daktari bingwa wa upasuaji wa uso katika hospitali hiyo Dokta Muammar A’araji amesema kuwa: “Vifaa tiba vilivyopo vimetusaidia kufanikisha upasuaji wa upande wa kulia wa uso wa kijana mwenye umri wa zaidi ya miaka thelathini kutoka mkoa wa Dhiqaar”.

Akaongeza kuwa: “Uvimbe ulibainishwa na mitambo ya maabara na tumeuondoa wote”. Akasema: “Hakuna maumivu yeyote aliyopata mgonjwa wakati wa upasuaji na tunatarajia afya yake itaimarika”.

Tambua kua hospitali ya rufaa Alkafeel hutoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa kila wakati, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: