Kuanza semina elekezi kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Idara ya maelekezo ya Dini chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kutoa semina elekezi kwa watumishi wa Ataba, kuhusu nyanja tofauti zinazo saidia kujenga uwezo wa watumishi, na kuwafanya wawezo kutoa huduma bora kwa mazuwaru, sambamba na utukufu wa wanaemtumikia.

Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Muhammad Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huu ni muendelezo wa semina zinazo fanywa na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya zinazo lenga kuboresha uwezo wa watumishi wake, na kuwafanya waweze kujibu maswali kwa ufasaha yanayo ulizwa na mazuwaru hususan yanayo husu Dini”.

Akaongeza kuwa: “Wakufunzi wa semina ni Masayyid na Mashekhe wanaotoa huduma katika kitengo cha Dini kwa kufuata ratiba maalum, wanasoma siku tano kila wiki, na kila siku ina zamu mbili, tunatarajia kufikia idadi kubwa zaidi ya watumishi, wanafundishwa mambo muhimu yanayo hitajika katika utekelezaji wa majukumu yao”.

Kumbuka kuwa Ataba tukufu inafanya kila iwezalo kuboresha uwezo wa watumishi wake, kitaaluma na kimaadili kulingana na kitengo cha kila mtumishi, semina hii ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: