Kumaliza upanuzi wa zaidi ya mita elfu moja

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wamemaliza kazi ya upanuzi wa mita za mraba (1450) katika haram, upande wa kushoto wa barabara ya Baabu-Qibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), sehemu hiyo imejumuishwa na sehemu zilizo tangulia kwa ajili ya kutumika katika kuhudumia mazuwaru.

Mhandisi mkazi bwana Ammaar Swalaah Mahadi msimamizi wa kazi hiyo, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi hiyo imejumuisha ujenzi wa (mfumo wa umeme – njia – mawasiliano – kamera – maji safi ya kunywa), kila mfumo umejengwa kama ilivyo pangwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya sambamba na kuweka ruva katika eneo lote za uwanja”.

Akafafanua kuwa: “Upanuzi huu umefanywa kwa awamu ya tatu katika haram hii takatifu, upo ndani ya mradi wa upanuzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, unaolenga kuongeza ukubwa wa eneo la Ataba tukufu pamoja na huduma zinazo tolewa kwa mazuwaru, na kupunguza msongamano hasa katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ukizingatia kuwa huu ni upande muhimu kwa watu wengi wanaokuja katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Kumbuka kuwa mradi huu unalenga kupunguza msongamano na kuongeza idadi ya mazuwaru, hususan kipindi cha ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ambazo huwa na msongamano hadi baadhi yao hushindwa kuingia ndani ya Ataba tukufu, hakika eneo hili hutumiwa na mazuwaru wengi, kutokana na umuhimu wa mlango huu katika nafsi za watu wanaokuja kumtembelea Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: