Mafunzo haya yanalenga kujenga uwezo wa vijana na kuendeleza vipaji vyao, wakufunzi ni wasomi waliobobea katika fani hiyo, watafundishwa mambo mbalimbali yanayo endana na umri wa washiriki ambao ni miaka (10 – 18).
Mada zitakazo fundishwa ni:
- - Kujiamini na uthubutu.
- - Mahadhi ya sauti.
- - Mahadhi ya lugha ya muili.
Aidha semina itakua na masomo ya Akhlaqi, Aqida na mengineyo, watafundishwa kwa nadhariyya na vitendo, vile vile kutakua na mijadala pamoja na majaribio, mwisho wa semina washiriki wote watapewa vyeti vya ushiriki na zawadi kwa watakao fanya vizuri.
Watakao faulu watapewa kipaombele cha kushiriki katika semina zingine na kuendeleza vipaji vyao ili kutengeneza kizazi cha wahadhiri bora.