Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel imeweka hema la mafunzo ya watu wanaojitolea kutoa huduma za afya

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut Akafeel chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya, imeweka hema la mafunzo la watu wanaojitolea kutoa huduma za afya, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na msimu wa huzuni za Husseiniyya, jumla ya watoa huduma (80) kutoka mkoa wa Basra na Dhiqaar wanashiriki kwenye mafunzo hayo.

Mkuu wa jumuiya ya Akaut kamanda Ali Hussein Abduzaidi amesema kuwa: “Lengo la semina hiyo iliyopewa jina la Imamu Jawaad (a.s) ni kutoa mafunzo kwa makundi ya watu wa kujitolea watakao toa huduma za afya katika ziara inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu, chini ya ratiba yenye vipengele vingi, kikiwemo kipengele cha afya, tabia, Aqida na mengineyo”.

Akaongeza kuwa: “Mafunzo yamedumu kwa muda wa siku tatu, wamefundishwa mbinu za uokozi, utoaji wa huduma ya kwanza kwa mgonjwa, na njia zinazo tumika kuokoa maisha ya mtu aliye katika hatali”.

Akabainisha kuwa: “Hema ni maalum kwa watu wanaojitolea kutoa huduma za afya”.

Kumbuka kuwa jumuiya ya Skaut Alkafeel chini ya kitengo cha Watoto na makuzi katika kitengo cha Habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu huwapa semina za mambo tofauti wanachama wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: