Alifiwa na watu sita wa familia yake katika tukio la moto la Nasiriyya.. kitu gani amesema?

Maoni katika picha
Tukio la kuungua kwa kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika hospitali ya Husseini mkoani Dhiqaar limeacha maumivu makali na visa vingi vya kuhuzunisha, ambavyo ni vigumu kuvisahau.

Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kutoa pole na kuwaliwaza waathirika wa tukio hilo, walikutana na tukio kubwa la kusikitisha, baba mmoja wa familia alifiwa na watu sita katika familia yake.. hicho ni moja ya visa vingi vya kuumiza katika tukio la kuungua kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mkoa wa Naswiriyya.

Shekh Wakiil anahadithia yaliyojiri baina yake na bwana huyo:

Baada ya kumaliza kuomboleza na kusimama ili tuombe ruhusa ya kuondoka, alisimama pembeni yangu mzee mwenye umri mkubwa, aliye umizwa zaidi na msiba huo na ukamuongezea uzee juu ya uzee na kuacha kidonda kikubwa katika roho yake.. akaanza kutuhadithia yaliyo mpata hadi akalia, sio rahisi kuona mtu mwenye umri kama wake analia, bali kubwa zaidi ni msimamo aliokua nao na umadhubuti wake.

Pamoja na maumivu makubwa aliyonayo lakini alikua imara.

Alikuwa na huzuni isiyo isha kwetu huenda kwa sababu alimkumbuka yule aliyejitolea nafsi yake kwa ajili ya kumlinda ndugu yake (kamanda wa Furaat).

Hatukua na chakufanya zaidi ya kumliwaza na kumpa pole pamoja na kusema.. hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

Mzee huyo (alifiwa na watu sita wa familia yake) alituhuzunisha sana, alituambia huku anafuta machozi yake kuwa: (Nifikishieni salamu kwa Hussein (a.s) na kwa Abbasi (a.s) hakika msiba wao ni mkubwa kushinda msiba wetu), kanakwamba aliishi au aliyaona madhila aliyopata Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s), kwa jinsi alivyo tuma salamu kwao na kujiliwaza kwa msiba wake.

Akamaliza kwa kusema: Kila anayesema kuwa raia wa Iraq wanamfano katika mapenzi na ikhlasi yao kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), nitamuambia: umechanganikiwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: