Kufungua mlango wa usajili katika semina ya upigaji wa picha kwa kutumia simu

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya imetangaza kuanza usajili wa kushiriki kwenye semina ya upigaji wa picha kwa kutumia simu, semina hiyo ni sehemu ya program ya kujenga uwezo awamu ya tano, inayolenga wavulana peke yake wenye umri wa miaka (10 hadi 18).

Semina inalenga kujenga uwezo wao na kubaini vipaji, msingi wa masomo hayo ni kauli isemayo (kipaji peke yake hakitoshi kuwa mpigapicha bora na kujifunza kwa wataalamu namna ya kufanya mambo ndio njia bora ya kuifanya kamera iongee bila maneno.

Mada za semina ni:

  • - Misingi ya upigaji picha.
  • - Makosa makubwa katika upigaji picha.
  • - Kanuni za muhimu katika upigaji picha.

Semina itakua na masomo tofauti ya Akhlaqi, Aqida na mengineyo.

Sifa za semina:

  • - Washiriki watapewa vyeti vya ushiriki baada ya semina.
  • - Washiriki watakaofanya vizuri watapewa zawadi.
  • - Mshiriki atapata mihadhara wakati wote na mahala popote atakapokua.
  • - Itatengenezwa toghuti maalum wakati wa semina itakayo tumika kufundishia na kutoa kazi na mitihani.

Watakao fanya vizuri kwenye semina hii watapewa nafasi ya kushiriki kwenye semina ijayo.

Ili kushiriki tuma taarifa zako kwenye telegram kupitia link ifuatayo @karrar_001.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: