Makamo katibu mkuu amesema: Kinacho fanywa na tawi la Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu kinastahiki pongezi

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussawi Ahmadi, ametembelea tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Najafu.

Ameangalia harakati na miradi ya Qur’ani pamoja na mikakati ya baadae, inayo lenga kufundisha utamaduni wa kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu sawa na malengo ya Atabatu Abbasiyya kwenye sekta hiyo.

Makamo katibu mkuu amepokewa na kiongozi wa tawi la Maahadi katika mkoa wa Najafu Sayyid Muhandi Almayali, aliye fafanua harakati na huduma zinazo tolewa na Maahadi, kama semina za makundi tofauti ya watu katika jamii, nadwa, warsha na vikao vya usomaji wa Qur’ani pamoja na kazi za kitafiti zinazo fanywa na watumishi wa tawi, ambapo hivi karibuni zaidi ya vitabu tisa vinavyo husu Qur’ani vitachapishwa.

Mwisho wa ziara hiyo makamo katibu mkuu alionyesha kuridhishwa na shughuli zinazo fanywa kwa ajili ya kutumikia vizito viwili Qur’ani tukufu na Ahlulbait (a.s), aidha amewashukuru watumishi wote wa tawi hilo na kuwataka waendelee kuchapa kazi.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Najafu ni moja ya matawi yanayo fanya vizuri kwenye sekta ya Qur’ani, linashughuli nyingi zinazo husu Qur’ani tukufu, ambazo zinachangia kuimarisha utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu katika sekta tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: