Ujumbe kutoka Ataba mbili tukufu umekuja kuwapa pole wahanga wa mlipuko uliotokea katika mji wa Swadri

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya unatoa pole kwa familia zilizo fiwa katika shambulio la kigaidi, lililotokea katika moja ya masoko ya mji wa Swadri mashariki ya mji mkuu wa Bagdad, jioni ya siku ya Idul-Adh-ha, ambapo watu 35 waliuwawa na makumi kujeruhiwa.

Ujumbe huo umejumuisha viongozi wa Ataba mbili na watumishi wake, wamewasilisha rambirambi za Marjaa Dini mkuu na viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba hizo pamoja na watumishi wa malalo hizo tukufu kwa familia za wafiwa na majeruhi.

Rais wa ujumbe huo na makamo katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya bwana Fadhil Auzu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara hii ni muendelezo wa ziara tunazofanya kwenye vituo tofauti, ziara ya mwisho ilikua ni kwenda kuwapa pole wahanga wa moto wa hospitali ya Imamu Hussein (a.s) katika mji wa Naswiriyya, ziara hizi zinafanywa chini ya maelekezo ya viongozi wakuu wa kisheria katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya”.

Akaongeza kuwa: “Tumekuja kuwapa pole wafiwa ambao ndugu zao wameuwawa bila kosa lolote katika tukio la kigaidi lililofanywa na watu wasio na ubinaadamu hata kidogo, tunawasilisha salamu na rambirambi kutoka kwa waheshimiwa viongozi wakuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na watumishi wa malalo hizo takatifu, kwa familia za mashahidi na raia wa Iraq kwa ujumla, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aziweke roho za mashahidi mahala pema peponi na awape subira na uvumilivu familia za wafiwa”.

Akafafanua kuwa: “Kuja kwetu kutembelea familia hizi ni sehemu ya mawasiliano kati ya Ataba mbili na jamii ya raia wa Iraq, ukiwemo mji wa Swadri ambao umekuwa mhanga mkubwa wa matukio ya kigaidi na kupoteza watu wengi, jinai hii ni muendelezo wa jinai nyingi zilizo wahi kutokea katika mji huu”.

Wafiwa walipongeza hatua hii na wakashukuru kwa kuja kuwapa pole na kuwaliwaza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: