Kuanza shindano la (Qutuuf) la kuhifadhi Qur’ani tukufu

Maoni katika picha
Idara ya Tahfiidh chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imetangaza kuanza kwa shindano la (Qutuuf) la kuhifadhi Qur’ani tukufu awamu ya kwanza, lenye vikosi nane kutoka mikoa tofauti ya Iraq, shindano hilo linafanywa ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Shindano hili ni kwa walio hifadhi juzuu tano za mwanzo, shindano linaangalia vipengele vingi, hasa kipengele cha uhifadhi bora, kukamilisha maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu, mpangilio wa kurasa na aya pamoja na kipengele cha maarifa ya uhifadhi na mambo mengine.

Kuna ushindani mkali baina ya washiriki, chini ya usimamizi wa jopo la majaji linalo undwa na Ustadh Alaau-Dini Alhamiri hukumu za usomaji, Ustadh Haafidh Qassim Haami ubora wa kuhifadhi, msomaji Haidari Jaluhani Mussawi sauti na naghma, katika mzunguko wa kwanza mchuano ulikua kati ya kundi la Shamiyya na Hindiyya, kundi la Hindiyya limeibuka na ushindi.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu Shekh Jawadi Nasrawi amesema: “Shindano hili ni muendelezo wa kazi za Maahadi ya Qur’ani tukufu katika kutumikia vizito viwili, kuna washiriki zaidi ya (24) wapo katika vikundi kutoka mikoa tofauti ya Iraq, nao ni wanafunzi wa Maahadi na matawi yake”.

Akaongeza kuwa: “Shindano hili ni sehemu ya maandalizi ya kushiriki kwenye mashindano mengine makubwa ya kitaifa na kimataifa, na kuwaweka tayali wakati wote, pamoja na kuwahamasisha wahifadhi Qur’ani yote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: