Muhimu: Huisha kiapo cha utiifu kwa kiongozi wa waumini (a.s) kwa niaba

Maoni katika picha
Idara ya Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuwa itafanya ziara maalum ya kiongozi wa waumini (a.s) katika kumbukumbu ya baiyya ya Ghadiir na sikukuu yake tukufu, pamoja na kuhuisha utii kwa kiongozi wa waumini (a.s) mbele ya malalo yake takatifu, katika siku ya Alkhamisi mwezi kumi na nane Dhulhijjah 1442h, kwa ajili ya wale watakao jisajili katika ukurasa wa ziara kwa niaba kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/.

Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hashim Shami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tunatoa huduma ya ziara kwa niaba ya kila aliyeshindwa kuja katika malalo ya kiongozi wa waumini (a.s), ziara na ibada za siku hiyo zitafanywa kwa niaba ya kila atakae jisajili katika ukurasa huo, kwa idhini ya mwenyezi Mungu mtukufu tutamfanyia ziara na kumswalia rakaa mbili pamoja na kumsomea dua, ibada hizo zitafanywa na mmoja wa watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) miongoni mwa Masayyid”.

Kiongozi wa idara ya taaluma za mitandao chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema: “Huduma ya kufanya ziara kwa niaba hutolewa na mtandao wa Alkafeel wakati wa ziara maalum, ikiwemo ziara ya siku ya Ghadiir, huwa tunatoa kipaombele maalum katika msimu huo, kutokana na idadi kubwa ya watu ndani na nje ya Iraq kushindwa kuja kufanya ziara wao wenyewe kwa sababu mbalimbali”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: