Mradi wa ujenzi wa magodauni awamu ya tatu na nne umekamilika chini ya usanifu wa kisasa unaoendana na sekta ya uchumi

Maoni katika picha
Mradi wa ujenzi wa magodauni awamu ya tatu na nne ni miongoni mwa miradi inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa lengo la kuhudumia sekta ya viwanda na kuondoa changamoto za kiuchumi, sambamba na uchumi wa dunia.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi Dhiyaau Swaaigh amesisitiza kuwa: “Mradi huu umejengwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa miradi muhimu inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ni mradi wa ujenzi wa magodauni maalum ya Ataba tukufu, yaliyopo katika barabara inayo unganisha mikoa miwili ya Najafu una Karbala, yamesanifiwa kisasa kila awamu imejengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (2m6000), na kila moja ina ghorofa mbili zilizo jengwa kwa usawa, eneo lote kwa ujumla linaukubwa wa (2m12000)”.

Akabainisha kuwa: “Magodauni yapo manne, kila moja linaukubwa wa (2m2500), ni majengo yaliyo pauliwa, yananguzo zenye urefu wa (mita 9.5), nguzo zilizo tumika ni aina maalum, huku sakafu ikiwekwa zege iliyo changanywa na Epoxy (kemekali inayo changanywa na kuwekwa juu ya zege kwa ajili ya kuimarisha sakafu na kuilinga na mipasuko au kushika uchafu), huku paa likitengenezwa kwa aina ya Space frame (mabomba ya chuma imara ambayo huunganishwa vizuri kama kenchi na kuwekwa paa juu yake) aina hii ya upauaji haitegemei nguzo katika ufungaji wa paa, mara nyingi hutumika katika ujenzi wa magodauni kwani huhitajika uwazi mkubwa ndani ya godauni usiokua na nguzo, kuna uwazi wa kiasi cha (2m25) bila nguzo, vifaa bora vya kisasa vimetumika katika ujenzi huu”.

Akaendelea kusema: “Mradi unamifumo kamili, ukiwemo mfumo wa zimamoto, utoaji wa tahadhari ya mapema, mfumo wa umeme, mfumo wa vyoo na mfumo wa ulinzi wa kisasa zaidi, aidha kuna mfumo wa kuzuwia mipasuko na mfumo wa simu, mfumo wa ngazi zinye uwezo wa kubeba hadi tani (5) nazo zimetengenezwa Ujerumani, pia kuta za magodauni haya ni imara sana na sakafu yake imewekwa marumaru maalum”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: