Iddi kubwa mbele ya Allah

Maoni katika picha
Siku ya mwezi kumi na nane Dhulhijjah, lilitokea tukio kubwa na tukufu, nayo ni sikukuu ya Ghadiir siku ambayo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipewa amri na Mwenyezi Mungu ya kumtangaza Ali bun Abu Twalib (a.s) kuwa khalifa na wasii na Imamu baada yake.

Kutokana na umuhimu wa jambo hilo Mwenyezi Mungu mtukufu alimuambia Mtume (s.a.w.w) awakusanye maswahaba na kuwafikishia ujumbe mara tu baada ya kufika eneo hilo, wala hakumuacha afike Madina, Mwenyezi Mungu anasema: (Ewe Mtume fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako na kama usipofanya utakuwa hujafikisha ujumbe wake, na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu, hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri).

Nayo ni siku tukufu, hadithi zimetaja utukufu wa siku hiyo, ambayo huchukuliwa kuwa tukio la pili kwa utukufu baada ya tukio la kupewa Utume na kushushwa Qur’ani takatifu, katika riwaya iliyo pokewa na Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu zake anasema: (Hakika siku ya Ghadiir inajulikana zaidi mbinguni kushinda aridhini).

Na imepokewa kutoka kwa Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu zake (a.s) anasema: (Anasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): Siku ya Ghadiir-Khum ni sikukuu bora katika umma wangu, nayo ni siku ambayo Mwenyezi Mungu mtukufu aliniamuru nimtangaze ndugu yangu Ali bun Abu Twalib (a.s) kuwa kiongozi wa umma wangu, atakaeongoza watu baada yangu, nayo ni siku ambayo Mwenyezi Mungu alikamilisha Dini na akatimiza neema kwa umma wangu, na akaridhia Uislamu kuwa Dini…).

Imeitwa kwa jina hili kwa sababu ya kukutana Mtume (s.a.w.w) na maelfu ya maswahaba wake wakati wakirudi kutoka hijja ya mwisho (hijjatul-widaa) katika eneo la kati ya Maka na Madina linalo itwa Ghadiir-Khum, hivyo siku ikaitwa kwa jina la sehemu.

Mwenyezi Mungu mtukufu alitimiza Dini yake na akakamilisha neema yake kwa waumini, kwa kutangazwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), kuwa khalifa, wasii na Imamu baada ya Mtume (s.a.w.w) katika siku ya Ghadiir-Khum, hivyo siku ya Ghadiir huchukuliwa kuwa sikukuu tukufu mno, hakuna Nabii yeyote aliyetumwa na Mwenyezi Mungu ispokua alisherehekea siku hiyo, kwa sababu ni siku ya kukamilisha Dini na kutimiza neema, neema gani kubwa zaidi ya kukamilika Dini, neema hii inastahiki pongezi na kumshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kuwaneemesha waumini katika siku hii tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: