Maukibu ya chuo kikuu cha Alkafeel inahudumia mazuwaru wa Idul-Ghadiir

Maoni katika picha
Maukibu ya chou kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inahudumia mazuwaru wanaokwenda kumzuru kiongozi wa waumini (a.s), katika kuadhimisha siku ya Ghadiir inayo sadifu leo siku ya Alkhamisi.

Maukibu hiyo ilianzishwa miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa rais wa chou, imekua ikihudumia mazuwaru kwenye matukio mbalimbali katika mkoa wa Najafu, likiwemo tukio hili tukufu, imeandaa na kugawa kiasi kikubwa cha maji safi ya kunywa na juisi, pamoja na vitu vingine, hayo ndio mahitaji makubwa ya mazuwaru kwa sasa kutokana na kuongezeka joto kwa kiwango kikubwa.

Maukibu imechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi katika utoaji wa huduma zake, kwa lengo la kulinda usalama wa mazuwaru na wahudumu wake, itaendelea kutoa huduma hadi msimu wa ziara utakapoisha.

Kumbuka kuwa huduma hizo zinalenga kuwapa kila wanacho hitaji mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: