Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya wanaadhimisha Ghadiir ya babu yao

Maoni katika picha
Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanaadhimisha sikukuu ya Ghadiir, siku ambayo alitangazwa babu yao kiongozi wa waumini Ali (a.s) na mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa amri ya Mwenyezi Mungu kuwa khalifa, wasii na Imamu baada yake.

Masayyid hao wamevaa nguo zao maarufu na kusimama katika milango ya haram takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kugawa mauwa kwa mazuwaru sambamba na kutoa pongezi kwa mwanae mbeba bendera ya Hussein Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku hii ambayo ilikamilika Didi na ikatimia neema, maua hayo ni ujumbe wa salamu na mapenzi makubwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).

Kumbuka kuwa kitendo hiki ni sehemu ya utamaduni uliozoweleka kwa masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu kila mwaka, pamoja na udogo wake lakini kinaonyesha ukubwa wa mapenzi yao kwa Ahlulbait (a.s) na mafungamano ya kiroho yaliyopo, wao ndio njia iliyonyooka iliyo husiwa na Mtume (s.a.w.w) kufuatwa, pia kitendo hicho cha utii hujenga furaha kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: