Mhadhara wa kuadhimisha Idul-Ghadiir katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa mhadhara wa kuadhimisha Idul-Ghadiir, asubuhi ya leo mwezi (18 Dhulhijjah 1442h) sawa na tarehe (29 Julai 2021m) ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na mazuwaru watukufu pamoja na wahudumu wa malalo hiyo takatifu.

Mhadhara umetolewa na Shekh Majidi Sultani, umefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha akaongea kuhusu utukufu wa siku hii na athari yake katika uislamu pamoja na kueleza umuhimu wa Idul-Ghaqiir na mchango wake katika Dini, sambamba na kula kiapo cha utii kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), akataja sifa nyingi na kuonyesha kuwa kuadhimisha Idul-Ghadiir ni kuhuisha alama kubwa ya uislamu, ambayo ni miongoni mwa alama alizohimiza Mwenyezi Mungu kuadhimishwa, hakika kufurahi na kusherehekea siku hii ni moja ya alama za kukubali Uimamu.

Kumbuka kuwa siku ya mwezi kumi na nane Dhulhijjah mwaka wa kumi hijiriyya alitangazwa Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) kuwa kiongozi wa waumini na khalifa wa Mtume (s.a.w.w).

Hivyo siku hiyo ni sikukuu tukufu mbele ya Mwenyezi Mungu na familia ya Mtume (a.s), Mwenyezi Mungu hakuwahi kutuma Nabii yeyote ispokua aliitukuza siku hiyo, siku hiyo mbingini inaitwa (siku ya ahadi iliyoahidiwa) na hapa ardhini inaitwa (siku ya ahadi iliyowekwa na kundi lililoshuhudia)
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: