Maktaba ya Ummul-Banina ya wanawake imeongeza uwezo wa maarifa tofauti zaidi ya elfu 20.

Maoni katika picha
Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, imeongeza vyanzo vya maarifa tofauti zaidi ya elfu (20).

Bibi Asmaa Ra’ad kiongozi wa maktaba hiyo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi hiyo ni sehemu ya mradi wa kuhakiki malengo na mikakati ya maktaba inayo lenga kuboresha huduma zinazo tolewa na maktaba, na kutoa fursa zaidi kwa wadau wake wanaokuja kusoma waweze kunufaika na vitabu vingi vya Maraajii pamoja na machapisho ya kisasa mbalimbali yanayo tolewa na watafiti wakubwa wa ndani na nje ya Iraq.

Akaongeza kuwa: “Tumeongeza zaidi ya vyanzo (14,900) na vitabu (60,000) vya kielektronik, huku tukiwa na vitabu (105) vya afya vilivyo andikwa katika lugha thelathini, vinavyo elezea mazingira na mambo mengine tofauti, sambamba na vitabu vya sheria ambavyo vipo vya nakala ngumu na laini (hard copy and soft copy)”.

Akabainisha kuwa: “Idara ya kuazimisha huchukua taarifa za nakala ngumu na laini pamoja na kuandaa program zinazo endana na mahitaji yao, ili kutoa huduma bora kwa wadau”.

Akamaliza kwa kusema: “Kunufaika na teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma za maktaba ni mafanikio makubwa kielimu, na moja ya njia ya kukuza huduma za maktana”.

Tambua kuwa jambo hili limefanywa na idara ya kusaidia usomaji kwa kushirikiana na idara ya uazimishaji katika maktaba ya Ummul-Banina (a.s) na maktaba ya chou kikuu cha Al-Ameed.

Kumbuka kuwa unaweza kupata huduma za maktaba kupitia toghuti ifuatayo: https://alkafeel.net/women_library/#/ au mitandao ya mawasiliano ya kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: