Pongezi za Ghadiir ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na Ataba zingine tukufu

Maoni katika picha
Katika kuadhimisha kutangazwa Imamu Ali (a.s) kuwa wasii na khalifa wa Mtume (s.a.w.w) katika Idi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Idul-Ghadiir, kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimealika wageni na kutoa zawadi za kutabaruku na siku hiyo adhim, ugeni huo umehusisha wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya, pamoja na viongozi wa Atabatu Alawiyya, Husseiniyya na Kadhimiyya.

Rais wa kitengo cha mahusiano Ustadh Muhammad Ali Azhar ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Miongoni mwa dira na malengo ya kitengo cha mahusiano ni kuimarisha uhusiano na kuadhimisha matukio ya kidini, miongoni mwa matukio hayo ni Idul-Ghadiir, watumishi wa kitengo chetu wameamua kutoa pongezi katika sikukuu hii, pamoja na maua yaliyo pambwa maneno mazuri ya kuadhimisha tukio hili”.

Akafafanua kuwa: “Program imehusisha wahudumu wa Ataba ya Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya na Abbasiyya, sambamba na kumuomba Mwenyezi Mungu akubali ibada zetu na atuimarishe katika wilaya ya kiongozi wa waumini (a.s) na alitunuku taifa hili kwa kulipa amani na utulivu na kuliepusha na kila aina ya balaa, awape nguvu wahudumu wa maeneo haya matakatifu za kuendelea kuhudumia mazuwaru watukufu”.

Wageni wamepokewa kwa maneno mazuri ya ukaribisho, na kumuomba Mwenyezi Mungu airudishe siku hii Iraq na raia wake wakiwa katika hali nzuri, atuondolee mabalaa na kila kinacho tatiza maisha ya raia wa taifa hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: