Pongezi za Idul-Ghadiir katika nyumba za familia za mashahizi

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetembelea familia za mashahidi katika mkoa wa Karbala, kwa ajili ya kuwapa pongezi na kushirikiana nao katika kusherehekea Idhul-Ghadiir, ambayo bado tupo katika siku zake.

Mkuu wa kituoa hicho bibi Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kituo kinaharakati nyingi katika makundi tofauti ya jamii, mara nyingi kwenye kila tukio la kidini huwa tunafanya moja ya harakati zetu, ikiwa ni pamoja na sikukuu ya Idul-Ghadiir, ambapo tumeona ni vizuri tukashirikiana na familia za wmashahidi katika kusherehekea sikukuu hii tukufu, tumeandaa kamati inayopita katika kila nyumba ya shahidi na kuwapa pongezi na zawadi za kutabaruku kutoka kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Kutembelea familia za mashahidi kunatupa mazingatio makubwa, shahada ni takrima ya Mwenyezi Mungu, hivyo tunasherehekea Idul-Ghadiir na familia zilizo jitolea kitu bora zaidi kwao kwa ajili ya taifa hili na maeneo matakatifu, pamoja na furaha ya siku hii lakini bado tunatakiwa kukumbuka damu takatifu iliyomwagika kwa ajili ya kutetea heshima na utukufu”.

Akamaliza kwa kusema: “Program hii imesaidia kuingiza furaha katika familia za mashahidi, na wameshukuru sana na wameomba tuendelee kuwakumbuka katika matukio mengine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: