Kuhitimisha shindano la (watafakari aya zake) la kuhifadhi Qur’ani kwa maudhui

Maoni katika picha
Kitengo cha masomo ya Qur’ani kwenye chou kikuu cha Ummul-Banina (a.s) cha wasichana katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimemaliza hatua ya mwisho ya shindano la (watafakari aya zake) linalo husika na kuhifadhi Qur’ani kwa maudhui, yaliyo fanywa wakati wa kuadhimisha Ghadiir ya Qur’ani isemayo kiongozi wa waumini Ali (a.s).

Hili ni miongoni mwa mashindano ya pekee, mashindano ya aina hii ni machache ndani na nje ya Iraq, shindano hili linaumuhimu mkubwa katika jamii na kwa muislamu mmoja mmoja, hususan kwa wale ambao ni vigumu kuhifadhi Qur’ani nzima kutokana na shughuli zao au kutokua na uwezo wa kuhifadhi.

Rais wa kitengo cha masomo ya Qur’ani Ustadh Ali Bayati ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hatua ya mwisho ya shindano hili ilikua na mahafidh (30) waliochujwa kutoka katika washiriki (250), na jopo la majaji waliobobea katika kuhifadhi Qur’ani kwa maudhui na tafsiri yake”.

Akaongeza kuwa: “Hili ni moja ya mashindano yanayo simamiwa na kitengo cha masomo ya Qur’ani, kwa lengo ya kufundisha masomo ya Qur’ani, Aqida, Hukumu na Akhlaq, kwa kuwataka washiriki wahifadhi aya zinazo zungumzia maudhui hizo, pamoja na kubainisha uhusiano wake kupitia tafsiri za Imamiyya”.

Akafafanua kuwa: “Shindano linawashiriki kutoka ndani na nje ya Iraq, kama vile Sirya, Lebanon, Kuwait na Saudia. Washindi wamepewa zawadi maalum, katika msimu ujao tunatarajia kupanua ushiriki wa shindano hili, baada ya muitikio mkubwa tulio shuhudia katika awamu hii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: