Kukamilika shindano la (Yaasubu-Dini) la Qur’ani

Maoni katika picha
Kitengo cha masomo ya Qur’ani katika chou kikuu cha Ummul-Banina (a.s) cha wasichana chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimekamilisha shindano la (Ya’asubu-Dini) linalohusu tafiti za kielimu.

Rais wa kitengo cha masomo ya Qur’ani Ustadh Ali Bayati ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano hilo lilifanywa mwishoni mwa mwezi wa Ramadhani, kwa lengo la kushajihisha uandishi wa tafiti zinazo husu Qur’ani, kitengo kilichagua mada mbili, ambazo ni:

  • - Mwenendo wa kufuata usia wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani kwa vijana wa kiislamu.
  • - Athari chanya ya kujifunza Qur’ani tukufu na kuhifadhi katika kuongeza elimu kwa wanajamii”.

Akaongeza kuwa: “Jumla ya tafiti zilizo shiriki zilikua (40) zikafuzu tafiti sita, (3) katika mada ya kwanza na (3) katika mada ya pili, tafiti zote ziliwasilishwa kwenye kamati ya majaji iliyofanya kazi ya kuzishindanisha na kupata zilizo shinda”

Akamaliza kwa kusema: “Shindano lilikua na washiriki kutoka ndani na nje ya Iraq kama Sirya na Saudia, washiriki wote watapewa vyeti vya ushiriki, na washindi watatu wa mwanzo katika kila mada watapewa zawadi pia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: