Kikao cha wawakilishi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vya Karbala

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimefanya kikao pamoja na wawakilishi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vya Karbala kwa ajili ya kujiandaa na mwezi wa Muharam mbele ya rais wa kitengo na wasaidizi wake, pamoja na wawakilishi wa vyombo vya usalama na utoaji wa huduma za kibinaadamu hapa mkoani.

Rais wa kitengo bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hiki ni moja ya vikao vingi vya maandalizi, vinavyo lenga kuweka mkakati wa pamoja kati ya kitengo na mawakibu na vikundi vya Husseiniyya, na kutengeneza mpango kazi utakaotumika, unao endana na maadhimisho ya Husseiniyya ndani ya mwezi wa Muharam, hususan katika kumi la kwanza ambalo linawahusu watu wa Karbala na mawakibu zao”.

Akaongeza kuwa: “Tumejadili mambo mengi yaliyo pendekezwa na wajumbe wa kikao, yanayo lenga kurahisisha shughuli za mawakibu Husseiniyya katika mazingira tuliyonayo, sambamba na kujadili mambo mengi yanayotakiwa kuzingatiwa na mawakibu, yatatangazwa kwa mawakibu zote siku jijazo”.

Akasema: “Tumejadili pia maswala ya usalama na utoaji wa huduma, na kusikiliza maoni ya wahusikua yanayo lenga kuwa na mpangilio mzuri utakao pelekea kuwa na maadhimisho salama”.

Akafafanua kuwa: “Kikao kimeweka maazimio mengi, ikiwa ni pamoja na kufanya maombolezo ya kifo cha Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kufuata maelekezo yote ya afya ya kujikinga na maambukizi, na kufuata ratiba iliyopangwa kwa kuzingatia muda wa kuingia na kutoka kila maukibu ya watu wa Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: