Maahadi ya Qur’ani tukufu imefanya semina ya Qur’ani na fani zake

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya kupitia tawi lake la Baabil inafanya semina yenye washiriki zaidi ya (18), kwa lengo la kusahihisha usomaji na kukuza uwezo wao katika usomaji wa Qur’ani.

Mkufunzi wa semina ni Dokta Muhammad Kadhim Ma’muri kutoka ofisi za Maahadi, anafundisha siku mbili kwa wiki, inatarajiwa kuendelea kwa muta wa miezi sita mfululizo, mada zinazo someshwa ni; naghma na usahihishaji wa makosa katika usomaji pamoja na sauti.

Tambua kuwa hii ni moja ya semina nyingi zinazofanywa na tawi la Maahadi kwa lengo la kuboresha usomaji wa Qur’ani tukufu na kuzingatia hukumu za tajwidi.

Kumbuka kuwa semina zinazo fanywa na Maahadi ya Qur’ani tukufu ni sehemu ya harakati zake, ambapo semina za Qur’ani ni moja ya harakati muhimu, Maahadi inatoa kipaumbele maalum kwa semina za Qur’ani kutokana na mafanikio makubwa yanayo patikana, kwa kupata wahitimu wengi wenye uwezo mzuri wa kusoma Qur’ani kwa kufuata hukumu za tajwidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: