Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimehitimisha semina ya usalama wa lugha ya kiarabu kwa watumishi wa hospitali ya Alkafeel.
Mkufunzi wa semina Dokta Majidi Nasoro amesema: “Semina imehusisha masomo ya lugha kwa ajili ya kusahihisha makosa ya kilugha na kinahau kwa watumishi, sawa iwe katika mawasiliano yao kazini au nyumbani kwenye Maisha yao ya kila siku”.
Akaongeza kuwa: “Lugha ya kiarabu inaumuhimu mkubwa kutokana na kufungamana kwake na ibada nyingi za kiislamu, washiriki wamevutiwa sana na semina hii, wameonyesha ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha semina”.
Akaendelea kusema: “Huu ni muendelezo wa semina nyingi wanazopewa watumishi wa hospitali ya rufaa Alkafeel kulingana na kitengo cha kila mtumishi, kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa kila mtumishi”.
Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hufanya warsha na semina mbalimbali kwa taasisi tofauti za Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kuongeza uwezo wao kiutendaji katika mambo mbalimbali.