Mafundi wa kitengo cha uhandisi wanaendelea na kazi ya ujenzi wa kituo cha tiba ya meno katika kitivo cha udaktari wa meno kwenye chou kikuu cha Al-Ameed.
Mhandisi mkazi Karari Barihi amewema: “Mradi huu ni maalum kwa ajili ya kufundisha wanafunzi hatua ya nne na tano kitivo cha meno katika chou kikuu cha Al-Ameed”.
Akaongeza kuwa: “Jengo litakua na wodi tano na ukumbi wa mapokezi, ni jengo la ghorofa tatu, kila moja inaukubwa wa mita za mraba (640)”.
Akaendelea kusema: “Hatua ya kwanza ilikua ya maandalizi, baada ya kupasishwa na viongozi wa chou, mafundi walianza ujenzi katika hatua ya pili, iliyo husisha ujenzi wa wodi na kuondoa mabaki ya ujenzi”.
Kasema: “Hii ni hatua ya tatu, inahusisha ujenzi na ukataji wa vyumba pamoja na upanuzi wa eneo kwa ajili ya kupokea idadi kubwa zaidi ya wagonjwa”
Kasisitiza kuwa: “Hatua ijayo tutaweka mifumo ya utoaji wa huduma na kufanya kazi za umaliziaji”. Akasema: “Hadi sasa kiwango cha ukamilifu kimefika asilimia %50”.
Kumbuka kuwa kitengo cha majengo ya kihandisi, kimesha kamilisha ujenzi wa kituo cha nje kwa wanafunzi wa udaktari wa meno katika chou kikuu cha Al-Ameed (jengo la Bayaariq Al-Ameed la kwanza).