Toleo hili linamada nyingi, miongoni mwa mada zake ni:
- - Fatuma Zaharaa (a.s) na nusra ya uislamu muhammadiyya/ Dokta Aamir Abduzaid Al-Waailiy.
- - Mazingatio katika kubainisha uwelewa wa kusubiri/ Mheshimiwa Sayyid Mahmuud Almuqaddasi Algharifi.
- - Turathi za kiaqida kwa Shia Imamiyya (utafiti wa Babaliyughurafiyya) kuanzia kwa Shekhe Swaduuq hadi kwa Allamah Hilliy.
- - Riwaya ya (Soma.. mimi sio msomaji) ni wahyi au uzushi?!/ Dokta Kaadhim Nasru-Llah.
- - Njia za kurekebisha jamii ya kiislamu kutokana na fikra za chuki za kisasa katika mtazamo wa Sayyid Shahidi Muhammad Baaqir, utafiti wa kidalili/ Dokta Baasim Abdulhussein Raahi Alhasanawi/ katoa nakala na mifano halisi.
- - Ubatili wa misingi ya falsafa ya kimagharibi katika mtazamo wa mitafizikia kwa watawala wa kwanza wa kiyunani/ Dokta Sanusi Saami.
Kumbuka kuwa jarida la (Al-Aqiida) ni miongoni mwa majarida yanayo tolewa na kituo, nalo huandika mambo ya Aqida na (Ilmu-Kalaam) ya zamani na sasa, kwa kuzingatia hoja za kiakili na dalili kutoka katika vizito viwili.