Waziri wa uhamiaji: Atabatu Abbasiyya tukufu inamchango mkubwa katika kuhudumia wakimbizi na kuwapa misaada

Maoni katika picha
Waziri wa uhamiaji wa Iraq bibi Iqaani Faaiq Jaabir amesema kuwa: Atabatu Abbasiyya tukufu inamchango mkubwa katika kuhudumia familia za wakimbizi wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh katika baadhi ya mikoa ya kaskazini, hakika Ataba ilikua msaada mkubwa kwa wizara.

Ameyasema hayo alipotembelea Atabatu Abbasiyya na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), akaongeza kuwa: “Atabatu Abbasiyya iligawa vitu vingi walivyo kuwa wakihitaji wakimbizi na kuwawekea mazingira ya kuishi salama katika kambi zao, msaada ambao ulifikia familia nyingi za wakimbizi”.

Akabainisha kuwa: “Sambamba na misaada iliyotolewa na Ataba tukufu, iliendelea kutoa huduma za kibinaadamu zilizo saidia kupunguza mateso kwa familia za wakimbizi na kuwafanya wavuke salama katika kipindi hicho, bila kusahau kazi kubwa iliyofanywa na Ataba tukufu katika wilaya ya Sanjaar”.

Akamaliza kwa kusema: “Ni Fahari kwangu kutembelea ardhi hii takatifu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hakika nimekua katika mazingira mazuri kiroho na nimehisi utukufu wa sehemu hii, jambo hili linaonyesha umoja wa raia wa Iraq bila kujali makundi na mitazamo yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: