Mwezi ishirini na nne Dhulhijjah ni siku ya Mubahala na kudhihiri nuru ulimwenguni

Maoni katika picha
Mwezi ishirini na nne Dhulhijjah ni siku ya mash-huud, ni msingi mkuu katika uislamu, ni siku ambayo nuru ya kiislamu iliangaza katika ujumbe wa Muhammadiyya, ni siku ya mash-huud iliyo thibitika ukuu wa maneno ya Mwenyezi Mungu, uislamu ukashinda, ukihadithiwa tukio la mwezi ishirini na nne Dhulhijjah utaona ukuu wa ujembe wa Muhammad, uliopatikana kupitia nafsi moja wala sio nyingi, mwanamke mmoja kutoka katika wengi, na Watoto wawili kutoka katika mengi, wote waja wema walioteuliwa na Mwenyezi Mungu na akawaandaa kuongoza umma baada ya Mtume wake (s.a.w.w).

Imepokewa katika riwaya kama ilivyo andikwa kwenye kitabu cha Tafsirul-Qummiy, kutoka kwa Swadiq (a.s) anasema: Wakristo wa Najrani walipo kwenda kwa Mtume (s.a.w.w), ulifika muda wa swala yao, wakaanza kupiga kengele na kuswali, maswahaba wa Mtume (s.a.w.w) wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu jambo hili linafanywa katika msikiti wako?! Akasema: Waacheni.

Walipo maliza kuswali wakasogea kwa Mtume (s.a.w.w), wakasema: Unalingania nini? Akasema (s.a.w.w): Nalingania shahada ya kwamba hakuna Mungu ispokua Allah na mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na hakika Issa ni mja aliyeubwa anakula, anakunywa na anaongea. Wakasema: Baba yake ni nani? Mtume (s.a.w.w) akashushiwa wahyi, akaambiwa: Waambie na nyie mnasema nini kuhusu Adam, je alikua ni mja aliye umbwa, anakula, anakunywa, anaongea na kuoa? Mtume akawauliza swali hilo. Wakasema: Ndio. Mtume (s.a.w.w) akasema: Nani baba yake? Wakakosa jibu, Mwenyezi Mungu akateremsha aya isemayo: (Hakika mfano wa Issa mbele ya Mwenyezi Mungu sawa na mfano wa Adam, aliumbwa kwa udongo kisha akauambia kuwa akawa..).

Halafu akashushiwa (s.a.w.w) aya isemayo: (Watakao kuhiji katika haya baada ya kukufikilia ilimu…) hadi (Tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo), hiyo ilikua ni amri ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume (s.a.w.w), akawaamia: Njooni tuapizane.. kama nikiwa mkweli laana itawashikia na kama mkiwa wakweli laana itanishukia. Wakasema: umesema vizuri. Wakakubaliana kuapizana na wakachagua siku ya kuapizana iwe mwezi ishirini na nne Dhulhijjah mwaka wa 10 hijiriyya.

Walipo rudi majumbani mwao, viongozi wao ambao ni Sayyid, Aaqib na Ahtam wakasema: Kama kwenye kuapizana akija na wafuasi wake tuapizane, atakua sio Mtume wa kweli, na akija na watu wa nyumbani kwake tusiapizane, hawezi kuja na watu wa nyumbani kwake ispokua ni mkweli. Walipo amka, Mtume (s.a.w.w) akaja na kiongozi wa waumini (a.s), Fatuma, Hassan na Hussein (a.s).

Ujumbe wa manaswara ukauliza: Wakina nani hawa? Wakaambiwa: Huyu ni mtoto wa Ammi yake na wasii wake Ali bun Abu Twalib, na huyu ni binti yake Fatuma, na hawa ni watoto wake Hassan na Hussein. Wakamuambia Mtume (s.a.w.w), Tumekubali, tunaomba tusiapizane.

Mtume akawakubalia na kuwataka walipe kodi (jazya), kila mwaka walipe jora elfu mbili za vitambaa na mwanamke mmoja pamoja na watoto wawili.

Hakika watu wote walio toka na Mtume (s.a.w.w) ni watukufu, walioteuliwa na Mwenyezi Mungu kuongoza umma huu baada ya Mtume (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: